Sera ya faragha
Rasimu, inasubiri mapitioHaya ni maandishi ya awali na yanaweza kubadilika kabla huduma haijazinduliwa.
e-Mialiko ni huduma ya EdSal Technologies ya kadi za mwaliko za kidijitali. Hapa tunaeleza kwa ufupi taarifa tunazotumia na kwa nini.
Taarifa tunazotumia
- Majina na namba za simu za wageni, kama wenyeji wa sherehe walivyotupa.
- Maelezo ya sherehe, na picha au muundo wa kadi wenyeji wakitupa.
- Majibu ya wageni (watahudhuria au la), hali ya ujumbe, na kadi zilizokaguliwa mlangoni.
Kwa nini
Kutuma mialiko na taarifa za sherehe hiyo tu, na kukagua kadi mlangoni. Hatuuzi taarifa, hatutumi matangazo, na hatuzitumii kwa sherehe nyingine.
Wanaotusaidia
- SMS zinatumwa kupitia NextSMS (NextByte ICT Solutions Co. Ltd, Dar es Salaam).
Muda wa kuhifadhi
- Majina na namba za wageni zinafutwa siku 90 baada ya sherehe.
Haki zako
Unaweza kuomba kujua taarifa tulizo nazo kukuhusu, kuzirekebisha au kuzifuta. Wasiliana nasi kwa njia zilizo hapa chini.
Wasiliana nasi
Kwa maswali kuhusu taarifa zako au masharti haya:
- info@emialiko.co.tz
- EdSal Technologies, Dar es Salaam, Tanzania